IQNA

Mapambano ya watu wa Bahrain

Mwanazuoni  mkuu  wa Bahrain asisitiza muendelezo wa Jihad, mageuzi

23:05 - December 18, 2022
Habari ID: 3476266
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi mkuu wa Kiislamu nchini wa Bahrain, Sheikh Isa Qassim amesisitiza kuendelea kwa njia ya Jihad na mageuzi katika nchi hiyo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.

Mwanazuoni huyo mwandamizi ametoa  maoni hayo, ambayo yalichapishwa kwenye akaunti yake rasmi ya Twitter, kwa mnasaba wa Siku ya Shahidi. Hii  ni siku ya wanafikra watukufu kufanya upya ahadi ya kuendeleza njia ya Jihad ili kuleta mageuzi na mageuzi, alisema.

Ayatullah Qassem ameongeza kuwa, Siku ya Shahidi inamkumbusha kila mtu kwamba kuuawa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni mafanikio makubwa zaidi, adhimu na yenye thamani kubwa katika maisha ya mwanadamu.

Pia alisisitiza umuhimu wa kuadhimisha Siku ya Mashahidi kama ishara ya kuinua vizazi kwa kuzingatia upendo wa kifo cha kishahidi kwenye njia ya Mwenyezi Mungu.

Siku ya Shahidi huadhimishwa katika nchi  hiyi ndogo ya kisiwa cha Ghuba ya Uajemi kila mwaka mnamo Desemba 17.

Siku hiyo inaadhimisha kuuawa shahidi kwa wanaume wawili Waislamu wa madhehebu ya Shia wakati mwamko  wa 1994 dhidi ya utawala wa Al Khalifa.

4107731

captcha